Klabu ya Yanga imekuwa ikitajwa katika tetesi kuhitaji saini za wachezaji wakubwa wa wapinzani wake Simba SC na Azam FC. Hii ni orodha ya wachezaji wakubwa waliowahi kuzitumikia timu za Simba na Azam Fc waliotajwa katika tetesi kutua Yanga na Yanga ikafanikiwa kupata saini zao.
1. Clatous Chama
Yanga ilikuwa na matamanio ya kumpata mwamba wa Lusaka kwa miaka mingi msimu huu wamefanikiwa kutimiza ndoto yao ya kupata saini mkali huyo wa soka kutoka Zambia. Clatous Chama alitambulishwa rasmi Yanga julai 1, 2024.
2. Prince Dube
Yanga ilimtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo (27) kutoka Azam FC kuelekea msimu ujao. Mchezaji wa kwanza kutambulishwa kujiunga na Yanga alikuwa ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia kutoka Simba SC.
3. Jean Baleke
Bado hajatambulishwa rasmi ila yupo katika kikosi cha Yanga katika Pre Sesoan maandalizi ya msimu ujao 2024/2025.
Klabu ya Yanga SC bado inatajwa pia kuwania usajili wa winga TP Mazembe (DR Congo), Phillipe Kinzumbi mwenye umri wa miaka 26.
Leave a Comment