Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WIZARA YA UJENZI NA WIZARA YA AFYA 12-02-2025

TANGAZO LA KUITWA KAZINI WIZARA YA UJENZI NA WIZARA YA AFYA 12-02-2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 25-05-2024 na tarehe 08-01-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

MUHIMU:

Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.

DOWNLOAD PDF HAPA CHINI

Leave a Comment