Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Maombi Vyuo Vya Afya: Jinsi ya Kuomba Chuo cha Afya 2025/2026

Maombi Vyuo Vya Afya: Jinsi ya Kuomba Chuo cha Afya 2025/2026

UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo mbalimbali utafunguliwa rasmi kuanzia Mei hadi Juni, 2025 katika awamu ya kwanza.

Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga kozi/programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Maombi ya kujiunga na kozi/programu mbalimbali yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

Aidha, Waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi – Tanzania Bara, wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) katika tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz).
Baraza pia, linawashauri waombaji, wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026 (Admission Guidebook for 2025/2026 Academic Year).

Baraza linatoa rai kwa waombaji wote kuandika taarifa zao sahihi na kutunza taarifa watakazopatiwa na Baraza bila kumpatia mtu yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi yao kujiunga na vyuo/ programu mbalimbali.

Leave a Comment