Fahamu Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Tanzania.
Sifa za mwombaji.
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
b) Awe na cheti cha kuzaliwa
c) Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA)
d) Awe na afya njema kimwili na kiakili
e) Asiwe na Kumbukumbu za Uhalifu
f) Awe hajaoa au kuolewa
g) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (Tatoos)
h) Awe hajawahi kutumia aina yoyote ya madawa ya kulevya
i) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
j) Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
k) Awe mwenye urefu usiopungua futi 5.7 kwa mwanaume na futi 5.4 kwa mwanamke
I) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
m) Umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Sifa za mwombaji.
a) Sifa zote zilizoainishwa kwenye Aya ya 1 (a hadi m)
b) Marubani wa Helikopta umri kuanzia miaka 18 hadi 35
c) Madereva, awe na leseni daraja E na umri kuanzia miaka 18 hadi 28 (watakaoitwa kwenye Usaili watafanyiwa uhakiki kwa njia ya vitendo, kuendesha magari makubwa)
Wenye Shahada.
Sifa za mwombaji.
a) Sifa zote zilizoainishwa kwenye Aya ya 1 (a hadi I)
b) Umri kuanzia miaka 18 hadi 28
Nyaraka Mhimu
a) Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
b) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
c) Fomu ya uthibitisho wa siha njema kutoka kwa mganga wa serikali
d) Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA
e) Picha ya Pasipoti ya hivi karibuni
f) Namba ya mtihani wa Kidato cha Nne
g) Namba ya mtihani wa Kidato cha Sita
h) Nakala ya vyeti vya kuhitimu elimu ya shahada au taaluma kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali
i) Barua ya Utambulisho kutoka kwa Afisa mtendaji wa Kijiji/mtaa.
Namna ya kufanya maombi.
Maombi yote huwasilishwa kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kikoa cha ajira.zimamoto.go.tz.
Leave a Comment