Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) anapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 18 Oktoba, 2024 hadi tarehe 19 Oktoba, 2024 kuwa majina ya
waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Aidha, ajira zao zitakuwa rasmi pale vyeti vyao vitakapohakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika. Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kwa kufika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) tarehe 27, 28, na 29 Januari, 2025 kuanzia saa tatu kamili asubuhi wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili zihakikiwe kabla ya kupewa barua ya ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa. Nyaraka za kuwasilisha ni kama ifuatavyo:
(i) Vyeti halisi (Original Certificates) na nakala mbili za vyeti hivyo zilizothibitishwa na Mamlaka za kisheria (certified by Advocate/Magistrate) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea;
(ii) Cheti cha kuzaliwa;
(iii) Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
(iv) Picha ndogo tatu za rangi (three colored passport size photographs)
PAKUA ORODHA HAPA CHINI
TANGAZO LA KUITWA KAZINI CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI (MUHAS) 13-02-2025
Leave a Comment