“Where Do You See Yourself in 5 Years?” ni moja ya swali linaloulizwa mara kwa mara katika usaili, unapoomba ajira. Swali hili ni sawa sawa na kukuuliza WHATS YOUR LONG TERM GOAL (kwenye kampuni yao). Anataka kujua, Je! Wewe ni mkaaji uu unapita tu? Anataka kujua kama utajidhatiti vipi na kazi, una malengo gani haswa kwenye kampuni.
Kuna kuna hatua muhimu unahitaji kufata wakati wa kujibu hili swali. Tutazipitia moja baada ya nyingine.
1. Unapotoa majibu yako weka connection kati ya malengo yako na maelezo(job descrption) pamoja na majukumu ya kazi.
2. Usionyeshe kuwa haujafikiria kuhusu malengo yako ya miaka mitano ijayo.
3. Usionyeshe kuwa huna nia ya kukaa muda mrefu katika kampuni au taasisi unayoomba kazi.
4. Kuwa mkweli.
Muhimu: Pangilia vizuri majibu yako. ukijibu kwa ujumla utafeli, mfano: “Mmmmh, I see myself as a manager, maybe with six figure salary scale and a lot of responsibilities.” Ukimaliza tu kujibu, jua tu hapo huna chako ndugu yangu, au ukijibu “I don’t know, a manager maybe.” Epuka matumizi ya “I DON’T KNOW, MAYBE , AM NOT SURE.
Leave a Comment