Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi (Application Letter) kwa Kiswahili. Barua ya maombi ya kazi yenye wasifu wako inaweza kumvutia mwajiri kutaka kupata maelezo zaidi kukuhusu, mafanikio yako na jinsi unavyoweza kufaidisha na kampuni yao au taasisi husika.

Waajiri wengi mara nyingi hutumia barua za maombi ya kazi ili kuchagua watu sahihi kabla ya kusonga mbele katika hatua ya usaili.

Vitu Mhimu vya Kuzingatia Unapoandka Barua ya Maombi ya Kazi

1. Kichwa cha habari (barua) kinachoeleweka

Hakikisha kichwa cha habari kinajitosheleza. Tumia maneno yanayotaja nafasi husika inayoombwa wazi wazi ili kumsaidia msomaji kujua unataka nini. Ni muhimu kutumia maneno yaliyo wazi na yanayoeleweka kwa urahisi kwa kuelewa kwamba mpokea maombi wakati mwingine hana muda wakufikiria ulichoandika.

Mfano,

‘YAH: KUOMBA KAZI YA ULINZI KATIKA KAMPUNI YAKO…’

Hapo inafahamika unataka nini moja kwa moja.

2. Onesha ulikopata habari za kazi unayoomba

Baada ya kuridhika na kichwa cha habari, ni muhimu sentesi inayoanza chini yake, kurejea tarehe ya tangazo la kazi unayoomba pamoja na namba ya kumbukumbu kama ipo au eleza ulivyosikia kuwepo kwa nafasi ya kazi.

Mfano, “Rejea tangazo lako la nafasi ya kazi lenye kumbukumbu namba XXX katika gazeti la Mtanzania la tarehe 24 Agosti 2014.”

Wengine wanapenda kuandika sentensi zisizo za lazima kama, “Kichwa habari hapo juu chakusika”. Ni mazoea tu lakini hulazimiki kuanza namna hiyo.

3. Sema wazi unaomba kazi na unaomba kazi gani

Baada ya kusema ulikopata habari za kazi unayoomba, tumia sentensi inayofuata kueleza nia yako ya kuomba kazi hiyo. Kumbuka msomaji wa barua hana muda wa kusoma maelezo yako mengi, ni muhimu kuandika kila kitu kwa kifupi na kwa uwazi.

Mfano, “Ninaandika barua hii kuomba kazi ya Ulinzi katika kampuni/shirika/taasisi yako kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo nililolitaja.”

4. Oanisha majukumu ya kazi na ujuzi ulionao

Kinachofuata katika aya zinazofuata ni kuonyesha namna unavyoweza kumudu majukumu yaliyotajwa kwenye tangazo hilo kwa kuyaoanisha na ujuzi na sifa za kitaaluma ulizonazo pamoja na uzoefu wa kazi ulionao. Mara nyingi majukumu ya kazi huainishwa katika tangazo la kazi hivyo ni muhimu sana kuonesha unavyokidhi majukumu hayo moja kwa moja.

5. Hitimisha kwa uungwana na ufasaha

Ni vyema kuhitimisha barua yako kwa kuonesha unavyofaa kwa kazi unayoiomba. Uchaguzi makini wa maneno kutakupa alama za ziada kuonyesha kwamba unajua kuwasiliana vizuri. Hakuna mwajiri angependa kuajiri mtu asiyejua kujieleza ipasavyo.

Mfano, unaweza kusema unatanguliza shukrani zako za dhati na kueleza kwamba uko tayari kuitwa kwa usaili. Unaweza kumaliza kwa kutaja nyaraka ulizoambatanisha pamoja na barua hiyo.

Mambo ya kuepuka

1. Kuandika vibaya Jina lako

2. Kuandika vibaya Jina la Kampuni

3. Kutofuata Maelekezo ya Tangazo la Kazi

4. Uandishi Mbovu (Poor Grammar)

5. Kuwasilisha Nyaraka (Documents) Zisizosahihi

DOWNLOAD PDF FILE (Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi)

Leave a Comment