Baadhi ya Vyuo Vinavyotoa Kozi ya Uuguzi (Nursing)
- Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili,
- Chuo kikuu cha St john cha Tanzania,
- Chuo kikuu cha St. Joseph
- Chuo cha sayansi ya afya Teofilo kisanji.
- Chuo kikuu – Mbeya,
- Chuo Kikuu cha Jimbo la Zanzibar,
- Chuo Kikuu cha Dodoma
- Chuo kikuu cha Zanzibar
Sifa Za Kujiunga Na Kozi ya Uuguzi (Nursing)
1.Kwanza kabisa, mwanafunzi anahitaji kuwa na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
2.Ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
3.Mbali na sifa za kitaaluma, sifa za kibinafsi pia ni muhimu katika uuguzi kama ilivyo kwenye kozi zingine za afya.
- Mwanafunzi anapaswa kuwa na upendo na huruma kwa wagonjwa,
- uwezo wa kufanya kazi kwenye timu,
- uwezo wa kusimamia mazingira ya dharura, na
- uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika hali ngumu.
Leave a Comment