Clinical Officer, au Clinical Medicine, ni mtaalamu wa afya ambaye ana ujuzi wa kufanya vipimo, kutibu na kutoa huduma za msingi za matibabu. Wao hufanya kazi kwa karibu na madaktari na wamepewa jukumu la kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
Kozi ya Clinical Medicine hutambulika kama ordinary diploma in clinical medicine. Kwa Diploma, muda wa masomo ni miaka mitatu na kupata cheti cha clinical assistant(CA)
Vyuo vinavyotoa Kozi ya Clinical Medicine/Clinical officer
- Clinical Officers Training Centre Mtwara – Mtwara
- Clinical Officers Training Centre Songea – Ruvuma
- Njombe Institute of Health and Allied Sciences (NIHAS) – Njombe
- Dental Therapists Training Centre Tanga – Tanga
- Mbeya College of Health Sciences – Mbeya
- Clinical Officers Training Centre Mafinga – Iringa
- Centre for Educational Development in Health Arusha – Arusha
- Clinical Officers Training Centre Maswa – Simiyu
- Clinical Officers Training Centre Lindi – Lindi
Sifa Za Kujiunga Na Kozi Ya Clinical Officer/Clinical Medicine
Kwa kuwa Clinical Medicine ni kozi muhimu sana katika fani ya afya, sifa za kujiunga nayo ni za kipekee. Mwanafunzi anahitaji kuwa na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) na kupata alama nne (4) katika masomo yasiyo ya dini, ikiwa ni pamoja na Kemia, Baiolojia, na Fizikia/ Sayansi za Uhandisi.
Pia, ni lazima awe na alama ya kufaulu katika Hisabati na Kiingereza. Hii itamwezesha mwanafunzi kujiunga na vyuo vinavyotoa kozi ya Clinical Medicine.
Leave a Comment