Kazi za Afisa Kilimo Msaidizi tanzania
i.Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio;
ii.Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio;
iii.Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora;
iv.Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti;
v.Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo;
vi.Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri;
vii.Kukusanya takwimu za mvua;
viii.Kushiriki katika savei za kilimo;
ix.Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za kutumia;
x.Kupanga mipango ya uzalishaji;
xi.Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi;
xii.Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo;
xiii.Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima;
xiv.Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu;
xv.Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;
xvi.Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo;
xvii.Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji;
xviii.Kutoa ushauri wa kilimo mseto;
xix.Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na;
xx.Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo
Mfano wa Barua ya Maombi ya Nafasi ya Afisa Kilimo Msaidizi
Mwandishi: Jina Lako
Anwani: S.L.P …………….
Simu: +255 7XX XXX XXX
Barua Pepe: jinalako1@email.com
Tarehe: XX.XX.XXXX
Kwa
Rasi wa Ndaki ya Kilimo
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
S.L.P 3000, Chuo Kikuu, Morogoro, Tanzania.
Yah: Maombi ya Nafasi ya Afisa Kilimo Msaidizi
Napenda kuwasilisha ombi langu la kazi kwa nafasi ya Afisa Kilimo Msaidizi kupitia tangazo la programu ya BBT-AEES. Nimehitimu Stashahada ya Sayansi ya Kilimo kutoka Chuo cha Kilimo, ambapo nimepata maarifa ya kina kuhusu uzalishaji wa mazao mbalimbali, hususani pamba.
Nikiwa na hamasa ya kusaidia jamii ya wakulima, nina uwezo wa kutoa ushauri juu ya kilimo bora cha pamba, na kuhakikisha kuwa kanuni za kilimo bora zinafuatwa kwa ufanisi. Pia, nina uzoefu wa kufuatilia na kuratibu matumizi ya pembejeo, pamoja na kusajili wakulima kwenye mfumo wa kidijitali.
Nimeambatanisha vyeti vyangu na wasifu wangu kwa ajili ya tathmini yenu. Niko tayari kufanya kazi kwa bidii na kujifunza zaidi kwa manufaa ya wakulima na maendeleo ya kilimo.
Wako mwaminifu,
[Jina Lako]
Leave a Comment