Kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani NA. 1 ya mwaka 2024 pamoja na Kanuni ya 12 (1) na (2) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za mwaka 2024, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kigamboni anawatangazia waombaji wote na nafasi ya Mwendesha Kifaa cha Bayometriki (BVR Operator) na nafasi ya Mwandishi Msaidizi waliochaguliwa kufika katika usaili utakaofanyika tarehe 01 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuanzia saa 2: 00 Asubuhi.
Waombaji wote wanatakiwa kuzingatia yafuatayo :-
· Muda wa kuanza usaili ni saa 2:00 Asubuhi
· Msailiwa atajigharamia gharama zote ikiwemo usafiri, chakula na malazi
· Fika ukiwa na kitambulisho chochote au barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mitaa.
· Kila msailiwa afike na cheti halisi cha kidato cha nne
Pamoja na tangazo hili imeambatishwa orodha ya majina ya waombaji waliochaguliwa.
Leave a Comment