Mwalimu Daraja la IIIA huyu ni mwalimu mwenye Astashahada (Cheti) ya Ualimu.
Sifa Kuu
Cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne na kufaulu mafunzo ya Ualimu ya miaka miwili (2) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali na kutunukiwa cheti cha Ualimu Daraja la IIIA.
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
Msharahara
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali anaanzia TGTS- B
Leave a Comment