Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Sifa Kuu za Kuajiriwa Tanzania

Sifa Kuu za Kuajiriwa Tanzania

Sifa za Jumla

i. Awe ni Mtanzania umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.

ii. Awe amehitimu shule, chuo au taasisi inayotambulika na Serikali.

iii. Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45) wakati wa kutuma maombi haya.

iv. Asiwe amewahi kuajiriwa. Waombaji waliostaafishwa au kufukuzwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Mambo ya Msingi ya Kuzingatia Unapoombna Ajira

1. Aambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

2. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

4. Maombi yote huambatanishwa na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
  • Computer Certificate
  • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVIKUBALIKI.

6. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

7. Zingatia tarehe katika kutuma maombi.

Hitimisho

Ajira za serikali maombi yote hufanyika kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.

Ajira zote hutangazwa kupitia kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira: https://www.ajira.go.tz/

Leave a Comment