Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza ajira mpya kwa vijana wa titanzania wenye sifa 2025. Fahamu utaratibu wa kufanya maombi ya ajira za Jeshi la Polisi Tanzania 2025.
1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.
2. Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi (https://ajira.tpf.go.tz).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa.
Leave a Comment