Fahamu vituo au Sehemu za Kufanyia Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025.
Sehemu ya Usaili Kwa wenye elimu ya kidato cha nne
Kwa waombaji waliomba ajira hizi kwa elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 09 Aprili, 2025 saa 1:00 asubuhi kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.
Sehemu ya Usaili Kwa Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali.
Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali usaili wao utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma kuanzia tarehe 14 Aprili hadi 17 Aprili, 2025, saa 1:00 asubuhi kwa kila kundi.
Leave a Comment