SHULE YA MSINGI S.L.P ……,
……………………….
TAREHE :…………………….
MWL. _________________________________
SHULE YA MSINGI
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA FEDHA (MHASIBU) WA SHULE.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteua kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo.
Kama mhasibu wa shule majukumu yafuatayo unapaswa kuyatekeleza:
i. Kuandaa vocha.
ii. Kuandaa hundi.
iii. Kuandaa taarifa ya mapato na matumizi.
iv. Kuandaa masuluhisho ya kibenki ( Bank reconciliation ).
v. Kuandaa taarifa ya robo mwaka.
vi. Kulipa posho mbalimbali za walimu.
vii. Kufanya kazi mbalimbali utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
viii.Kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo fedha.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment