SHULE YA MSINGI ……
S.L.P ……..,
TAREHE :…………………..
MWL………………………………………………………………………….
SHULE YA MSINGI.
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA MICHEZO WA SHULE
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo.
Kama mwalimu wa michezo unatakiwa kutekeleza majukumu yafuatayo:
i.kupanga,kupanga na kusimamia michezo yote shuleni.
ii.kuhakikisha uwepo wa viwanja vyote vya michezo shuleni.
iii.kuratibu mashindano ya michezo mbalimbali shuleni.
iv.kupanga bajeti ya vifaa vya michezo shuleni.
v.kuhamasisha michezo shuleni.
vi.kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo michezo shuleni.
vii.kufanya kazi zingine utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment