Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Barua ya Kuteuliwa Kuwa Mwalimu wa Nidhamu na Malezi wa Shule

Barua ya Kuteuliwa Kuwa Mwalimu wa Nidhamu na Malezi wa Shule

SHULE YA MSINGI S.L.P ………..,
TAREHE :___________________
MWL :__________________________

YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA NIDHAMU NA MALEZI WA SHULE

Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa nidhamu unapaswa kufanya majukumu yafuatayo:

i. kuhimiza nidhamu bora na maadili kwa wanafunzi.

ii. kuandaa sheria,taratibu na kanuni za shule na kuzisimamia kikamilifu.

iii. kutoa ushauri kwa wanafunzi na wazazi juu ya mambo mbalimbali ya kitabia.

iv. kuwaelimisha wanafunzi mara kwa mara juu ya wajibu na haki zao kufuatana na kanuni na taratibu za shule.

v. kuweka kumbukumbu za adhabu zinazotolewa na walimu shuleni na kupeleka kwa mwalimu mkuu.

vi. kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo nidhamu kwa wanafunzi.

vii. kushughulikia tuzo za zawadi mbalimbali shuleni.

viii. kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.

Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.

Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.

Wako katika utumishi.
………………………………

Leave a Comment