Majina Walioitwa Kwenye Usaili wa Oral TRA 2025: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwataarifu wasailiwa wote waliofanya usaili wa kuandika tarehe 29 na 30 Machi, 2025 katika vituo tisa (9) vilivyokuwa vimeandaliwa hapa Nchini kwamba matokeo ya usaili huo yamekamilika na yanapatikana katika Tovuti ya Mamlaka.
Matokeo hayo yanaonesha namba ya mtihani na matokeo aliyopata msailiwa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inawashukuru wasailiwa wote kwa kuonesha nia ya kuitumikia Mamlaka na kuwatakia kila la kheri wote waliofaulu na kuchaguliwa kwenda katika hatua zinazofuata.
Leave a Comment