Sample ya Barua ya Maombi Ajira Jeshi la Wananachi Tanzania JWTZ 2025

Mfano wa Barua ya Maombi Ajira Jeshi la Wananachi Tanzania JWTZ 2025.

Mwajuma Mwenda
P.O.BOX 12
0712345678
Ubungo
Dar es salaam
31/04/2025

Mkuu wa Utumishi Jeshini
Makao Makuu ya Jeshi
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, TANZANIA.

Mheshimiwa,

YAH: Maombi ya Nafasi ya Kujiunga na JWTZ – Askari

Ninaandika barua hii kuomba nafasi ya kujiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Nimepata taarifa kuhusu nafasi hii kupitia tangazo lililotolewa na luteni kanali kaimu mkurugenzi wa habari na uhusiano makao makuu ya jeshi JWTZ kwenye tovuti rasmi.

Nimekuwa nikitamani kujiunga na JWTZ tangu nilipokuwa mdogo, nikivutiwa na nidhamu, uzalendo, na kujitolea kwa wanajeshi wetu. Ninaamini kuwa kujiunga na JWTZ kutanifanya niwe raia bora zaidi na kunipa fursa ya kuchangia katika ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Nimemaliza elimu yangu ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kizuka mwaka 2023 na kupata ufaulu wa daraja la II na kisha kujiunga na mafunzo ya JKT mujibu wa sheria katika kambi ya JKT Ruvu.

Wakati wa masomo yangu, nilikuwa kiongozi katika klabu ya michezo na pia nilipata mafunzo ya msingi ya kompyuta. Nina afya njema na ninajiamini kuwa nina uwezo wa kukabiliana na changamoto za mafunzo ya kijeshi.

Ninaamini kuwa nidhamu yangu, uwezo wangu wa kujifunza haraka, na ari yangu ya kutumikia nchi vitanifanya niwe rasilimali muhimu kwa JWTZ. Nitafanya kazi kwa bidii na kujitolea kikamilifu katika majukumu yangu.

Nimeambatanisha nakala za vyeti vyangu vya elimu, cheti cha kuzaliwa, na picha ya pasipoti kama inavyotakiwa. Ningependa kupata fursa ya kuhojiwa ili niweze kuelezea zaidi nia yangu na sifa zangu.

Nakushukuru kwa kuzingatia maombi yangu.

Wako Mtiifu,

[Sahihi Yako] Mwakipesile Ndyamana

DOWNLOAD PDF HAPA

Leave a Comment