Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wahusika wote wanatakiwa kufika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 18 Mei, 2025 bila kukosa; kwa ambaye hatafika chuoni kwa tarehe zilizopangwa hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.
Kufika chuoni shuka kituo cha Kabuku kilichopo kilometa 12 toka chuoni. Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea kwa tarehe zilizotajwa hapo juu, kuanzia
saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.
Mhusika atapaswa kujigharamia nauli ya kwenda sambamba na chakula na malazi kwa siku zote ambazo atakuwa hajapokelewa Chuoni. Mhusika anapaswa kuja akiwa na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioombea pamoja na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba na leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva. Vyeti vyote tajwa hapo juu viwe na nakala tatu kwa kila cheti pia vyeti hivyo vitakaguliwa na kwa ambaye majina yake yatatofautiana kati ya vyeti vya shule/taaluma, NIDA na cheti cha kuzaliwa watarudishwa na nafasi zao zitachukuliwa na wengine.
Mhusika atakapofika chuoni awe tayari kupimwa afya ya mwili, akili na Mimba kwa wanawake na ambaye atabainika kuwa na kasoro za kiafyahataruhusiwa kuendelea na
mafunzo na atarudishwa kwa gharama zake na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.
Wahusika wote wanatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo: mashuka mawili (02) ya rangi ya bluu, mto 01 na foronya 02 ya rangi ya bluu, chandarua 01 rangi ya bluu (cha duara), ndoo ya plastiki ya lita 20, sahani na kikombe cha bati, fedha kiasi kwa matumizi binafsi na bima za afya kwa walionazo. Aidha vifaa vifuatavyo watanunua kwenye duka la Chuo, raba za michezo, fulana (T-shirt) rangi ya bluu, Madaftari makubwa (counter books 4 quire 5 pcs), vifaa vya michezo (truck suite, bukta bluu, na fulana) na kalamu.
Leave a Comment