Mahitaji ya Kupata Leseni ya Udereva kwa Mara ya Kwanza
Ili kupata leseni ya udereva kwa mara ya kwanza, unahitaji kutimiza mahitaji yafuatayo:
- Umri: Kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi kwa magari na miaka 16 au zaidi kwa pikipiki.
- Mafunzo: Hudhuria mafunzo katika chuo kinachotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upate cheti cha kuhitimu.
- Leseni ya Kujifunza: Pata leseni ya kujifunza (provisional) kutoka TRA.
- Mtihani wa Nadharia: Fanya na ufaulu mtihani wa nadharia kuhusu sheria za barabarani na usalama.
- Mtihani wa Vitendo: Fanya na ufaulu mtihani wa vitendo wa kuendesha gari.
- Cheti cha Afya: Pata cheti cha afya kutoka kwa daktari kinachothibitisha kuwa una afya nzuri ya kuendesha gari.
- Malipo: Lipa ada zote zinazohitajika kwa TRA.
Majaraja ya leseni za udereva
Tanzania ina madaraja mbalimbali ya leseni za udereva, kulingana na aina ya gari unayotaka kuendesha:
- Daraja A: Pikipiki (za ukubwa tofauti)
- Daraja B: Magari ya binafsi
- Daraja C: Magari ya abiria (daladala, mabasi)
- Daraja D: Magari ya mizigo
- Daraja E: Magari yote (isipokuwa ya abiria na pikipiki)
- Daraja F: Mitambo maalum (forklifts, graders)
- Daraja G: Mitambo ya kilimo na migodi (tractors)
- Daraja H: Leseni ya kujifunza (provisional)
Leave a Comment