SHULE YA MSINGI S.L.P …………,
TAREHE ………………..
MWL :_____________________________
SHULE YA MSINGI
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA AFYA NA MAZINGIRA.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu, napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa mazingira una wajibu wa kutekeleza yafuatayo:
i.kuhamasisha na kufuatilia utunzaji wa mazingira shuleni.
ii.kusimamia ukarabati wa samani mbalimbali za shule.
iii.kuhakikisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ni salama na rafiki shuleni.
iv.kuhakikisha shule inapangwa mawe na kupakwa chokaa.
v.kuhamasisha wanafunzi upandaji wa maua na miti shuleni.
vi.kuhakikisha mazingira ya shule ni safi na yanavutia.
vii.kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
viii.kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo mazingira ya shule.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment