SHULE YA MSINGI
S.L.P 10,
TAREHE ………………………..
MWL …………………………………………………
SHULE YA MSINGI
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA DARASA LA ……………………
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteua kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa darasa unapaswa kutekeleza majukumu yafuatayo katika darasa lako:
i. Utakuwa mlezi wa darasa.
ii. Kupitia na kutunza daftari la mahudhurio ya wanafunzi ( attendance register)
iii. Kupitia na kusaini shajala la somo katika darasa lako .
iv. Kutoa taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi kwa mwalimu wa zamu.
v. Kupokea na kusikiliza shida za wanafunzi katika darasa lako na kuzitatua.
vi. Kuwaelewa kikamilifu wanafunzi katika darasa lako ili kutoa ushauri kuhusu maendeleo yao ya kila siku .
vii. Kuhakikisha kuwa ratiba ya masomo, usafi na chati ya masomo zinabandikwa kwenye mbao za matangazo darasani.
viii. Kusimamia uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi katika darasa lako.
ix. Kutunza kumbukumbu za maendeleo ya masomo na mwenendo wa tabia za wanafunzi darasani.
x. Kujaza na kutuma taarifa za maendeleo ya wanafunzi kwa wazazi au walezi kila mwisho wa muhula na kushauriana nao .
xi. Kufunga taarifa ya kila mwezi kwenye daftari la mahudhurio ya wanafunzi .
xii. Kudhibiti utoro wa wanafunzi katika darasa lako .
xiii. Kutoa ruhusa mbalimbali za wanafunzi darasani kwako .
xiv.Kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo darasa lako .
xv. Kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment