SHULE YA MSINGI S.L.P ……,
……………………………
TAREHE :……………………
MWL______________________________
SHULE YA MSINGI
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA MAAFA NA STAREHE WA SHULE
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa maafa na starehe una wajibu wa kutekeleza yafuatayo:
i. kuratibu na kusimamia mambo yote yanayohusiana na maafa na starehe shuleni.
ii. kukusanya michango yote inayohusiana na maafa na starehe na kuiwasilisha sehemu husika bila kuchelewa.
iii. kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo maafa na starehe.
iv. kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.]
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment