Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Barua ya Kuteuliwa Kuwa Mwalimu wa Taaluma wa Shule

Barua ya Kuteuliwa Kuwa Mwalimu wa Taaluma wa Shule

SHULE YA MSINGI ……………,

S.L.P ………..,

KASULU.

TAREHE ……………………………….

MWL…………………………………………

SHULE YA MSINGI MURUSI.

YAH:KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA TAALUMA SHULENI.

Husika na kichwa cha habari hapo juu , kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteua kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo.

Kama mwalimu wa taaluma unatakiwa kutekeleza majukumu yafuatayo:

i. Kupanga,kuratibu na kusimamia taaluma shuleni.

ii. Kufuatilia ufundishaji shuleni pamoja na kutoa ushauri kwa walimu juu ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi.

iii. Kupanga,kuratibu na kusimamia uendeshaji wa mitihani yote ya nje na ndani shuleni.

iv. Kutathmini mitihani yote ya kitaifa ili kubaini mafanikio na udhaifu ili kurekebisha mapungufu hayo.

v. Kufuatilia upotevu wa vipindi darasani.

vi. Kutekeleza maagizo yote utakayopangiwa na mwalimu mkuu.

vii. Kutunza kumbukumbu zote zinazohusiana na taaluma shuleni.

viii. Kuhakikisha ratiba kuu ya masomo shuleni imeandaliwa na kubandikwa katika ofisi zote.

ix. Kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo taaluma shuleni.

x. Katibu wa vikao vya taaluma shuleni ambavyo vinaunganisha wakuu wa idara zote za masomo. Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.

Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.

Wako katika utumishi.
……………………………

Leave a Comment