SHULE YA MSINGI S.L.P …..,
TAREHE :………………….
MWL :_____________________
SHULE YA MSINGI .
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA MIRADI (EK) WA SHULE
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo.
Kama mwalimu wa miradi unapaswa kutekeleza majukumu yafuatayo:
i.kupanga na kuratibu shughuli zote zinazohusiana na miradi ya shule.
ii.kuhakikisha shule ina eneo la kutosha kwa ajili ya kilimo.
iii.kuandaa mapato na matumizi ya miradi yote ya shule.
iv.kuhamasisha kilimo cha kisasa shuleni.
v.kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
vi.kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo miradi ya shule.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment