SHULE YA MSINGI , S.L.P ……..,
…………………………
TAREHE ………………………….
MWL ……………………………………………….
MURUSI SHULE YA MSINGI.
YAH:- KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA VIFAA NA TAKWIMU WA SHULE
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteuwa kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa vifaa na takwimu unapaswa kutekeleza majukumu yafuatayo:
i.kupanga na kuratibu shughuli zote zinazohusiana na takwimu za shule.
ii.kukusanya,kuchambua,kufafanua,kuhifadhi,kutoa na kupokea vifaa vyote na kuwasilisha zinapohitajika bila kuchelewa.
iii.kusimamia zoezi la uazimishaji wa vifaa vyote shuleni.
iv.kutunza na kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na takwimu za shule.
v.kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
vi.kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo takwimu za shule.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment