CV na Profile ya Kocha Mpya wa Simba: Fadlu Davids (43) ni raia wa Afrika Kusini alikuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco. Uongozi wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili.
CV ya Fadlu Davids
Fadlu Davids ana Leseni ya Uefa Pro Licence, anapendelea mfumo wa 4-2-3-1. Msimu wa mwaka 2018/19 na 2021/22 alikuwa kocha msaidizi wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, msimu wa 2022/23 alikuwa kocha msaidizi wa Locomotiv Moscow ya Russia, msimu wa 2023/24 alikuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco.
Davids ameshakuwa kocha mkuu mara kadhaa akiwa na kikosi cha Orlando Pirates pamoja na Martizburg United zote za Afrika Kusini.
Simba SC chini ya Fadlu Davids
Simba ndani ya msimu wa 2024/25 kwenye ligi baada ya kucheza mechi 15 imekusanya jumla ya pointi 40 ikiwa namba moja huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 31 ikiwa ni namba mbili kwa timu zenye mabao mengi.
Leave a Comment