Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
DIRISHA LA KUBADILISHA TAHASUSI KWA MWAKA 2025

DIRISHA LA KUBADILISHA TAHASUSI KWA MWAKA 2025

TAMISEMI imekuwa inawapa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kubadili au kuweka machaguo mapya ya shule, chuo au tahasusi pale matokeo yanapotoka ili kumpa nafasi mwanafunzi kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wake (CSEE). Makala hii inakupa mwongozo jinsi ya kutumia mfumo huo wa Tamisemi.

Mwanafunzi (Muhitimu wa Kidato cha Nne (Form Four)) – Jukumu lake kuu katika mfumo wa Selform ni kubadilisha baadhi ya taarifa binafsi kama Home AddressMobile Number, Email Address na machaguo ya shule, vyuo na tahsusi zake katika seksheni zingine kutokana na ufaulu katika matokeo yake.

NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA SELFORM

Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili kama inavyoonekana hapo chini. Bofya Menu ya chini kabisa iliyoandikwa For Candidates, Click here to Register kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Kisha, ujaze taarifa zinazohusika za Index Number kwa format ya Mfano S0101.0020.2018, Jibu swali utakaloulizwa, Jina la Ukoo na Mwaka wa kuzaliwa kama inavyoonekana hapo chini.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Kisha dirisha litafunguka na kutaka ujaze Password utakayoitumia siku zote. Dirisha lifuatalo litafunguka;

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Ukishaandika Password, mfumo utaonekana katika sura hii kuonesha umefanikiwa kubadili Password;

Ukishabadili Password, utaitumia kuingia kwa mara nyingine kwa kuandika username

mfano S0101.0002.2018 na Password uliyoibadili.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

PART A: TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI

Ukishaingia kwenye mfumo, dirisha lifuatalo litafunguka na sehemu zilizozungushiwa tu ndio utaweza kubadili taarifa binafsi. Ukimaliza kujaza bofya Save and Next hapo chini ili kuendelea mbele.

C:\Users\mtatifikoloj\Downloads\Capture 2019-03-27 at 19.10.04.png

PART B1: STUDENT GENERAL CHOICES

Bofya katika sehemu hii ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo.

PART B2: ALTERNATIVE OPTIONS

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya vyuo vya Kisekta. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT.

PART C1: FORM V STUDENT DETAILED CHOICES

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya shule za form V na tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi ataona Possible combinations tu na shule kutokana na ufaulu wa matokeo yake kwa lengo la kubadilisha. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C2: TECHNICAL EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Technical na Tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa Tahsusi ya PCM katika matokeo yake kwa ajili ya kubadilisha eneo hili. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C3: HEALTH EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Afya na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C4: DIPLOMA EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Elimu na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C5: OTHER COLLEGES

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo Vinginevyo na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

VIDEO

BONYEZA HAPA KUANZA KUBADILI

Leave a Comment