Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi za kazi 1,596 katika fani mbalimbali kuanzia tarehe 06 hadi 19 Februari, 2025, ambapo maombi ya kazi 135,027 yalipokelewa.
TRA imepitia kwa umakini mkubwa maombi yote yaliyopokelewa na kupata waomba kazi 112,952 waliokidhi vigezo vilivyowekwa na hivyo kustahili kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika (Written Interview) ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 Machi, 2025.
Leave a Comment