Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa Tigo Pesa
- Ingiza *150*01# kwenye simu yako kisha piga.
- Chagua “Lipia Bili.”
- Chagua nambari 2 kupata majina ya kampuni.
- Chagua namba 5 “King’amuzi.”
- Chagua namba 2 “StarTimes.”
- Chagua namba 1 “Weka namba ya kumbukumbu.”
- Ingiza namba ya kumbukumbu ambayo ni Smartcard namba ya king’amuzi chako.
- Ingiza kiasi kamili cha kifurushi unachotumia.
- Ingiza namba yako ya siri kuhakiki.
- Utapokea ujumbe kuthibitisha muamala wako wa malipo.
Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa M-Pesa:
- Ingia kwenye Menu ya M-PESA kwa kupiga *150*00#.
- Chagua namba 4 “Lipia Bili.”
- Chagua “StarTimes” kwenye orodha.
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (Smartcard namba).
- Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kulipia.
- Ingiza nambari yako ya siri ya M-Pesa ili kuhakiki muamala.
Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa Airtel Money:
- Piga *150*60#
- Chagua 5 – Lipia bili
- Chagua 6 – King’amuzi
- Chagua 2 – StarTimes
- Ingiza namba ya smartcard
- Weka kiasi
- Thibitisha kwa kuingiza PIN yako

Leave a Comment