Cover Letter ni nini?
Cover Letter ni sawa na kusema barua ya maombi ya kazi ambayo unawasilisha kama sehemu ya maombi yako ya kazi, pamoja na wasifu wako au CV.
Madhumuni ya Cover Letter ni kukutambulisha na kufupisha kwa ufupi historia yako ya kitaaluma. Kwa wastani, inapaswa kuwa na urefu wa maneno 250 hadi 400.
Cover Letter nzuri inapaswa kumvutia HR na kuwashawishi kuwa unastahili kuitwa katika usaili wa kazi uliyoomba.
Sehemu Mhimu katika Cover Letter
Kichwa. Ongeza maelezo yote muhimu ya mawasiliano juu ya barua yako ya kazi.
Salamu rasmi. Chagua njia inayofaa ya kusalimia hadhira unayolenga.
Utangulizi. Jitambulishe katika aya ya mwanzo na ueleze nia yako.
Kiini. Eleza kwa nini wewe unafaa kufanya kazi katika kampuni. Lenga “kuuza” ujuzi wako, mafanikio, na uzoefu wa kitaaluma unaofaa.
Hitimisho. Fanya muhtasari wa mambo yako muhimu na uyamalize kitaalamu.
Sample

Leave a Comment