Kuna njia kuu mbili za kuangalia matokeo ya kidato cha nne kutoka baraza la Mitihani NECTA, ambazo ni kupitia SMS na Mtandaoni. Kupitia makala hii utafahamu njia zote mbili, soma hadi mwisho.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Mtandaoni
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA anwani: www.necta.go.tz.
2. Chagua Sehemu ya “Results” (Matokeo ya Mitihani)
Baada ya kufungua tovuti, bofya kitufe cha Results kinachoonekana kwenye menyu kuu. Hii itakufikisha kwenye orodha ya mitihani yote inayosimamiwa na NECTA.
3. Chagua “CSEE” (Certificate of Secondary Education Examination)
4. Chagua Mwaka wa Mtihani
Baada ya kufungua ukurasa wa CSEE, utaona miaka ya matokeo iliyoorodheshwa. Tafuta na chagua mwaka husika, yaani, 2024.
5. Tafuta Jina la Shule
Mara baada ya kuchagua mwaka, utaelekezwa kwenye orodha ya shule zote zilizoshiriki mtihani huo. Tumia kipengele cha utafutaji kutafuta jina la shule yako ili kuonyesha matokeo ya wanafunzi wote wa shule hiyo.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Kupitia Mfumo wa SMS
1. Fungua sehemu ya kuandika ujumbe kwenye simu yako.
2. Andika ujumbe huu: CSEE ikifuatiwa na namba ya mtihani wa mwanafunzi (mfano: CSEE 12345678910).
3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15300.
4. Utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo ya mwanafunzi mara tu ujumbe wako utakaposambazwa na kupokelewa.
Leave a Comment