NECTA imejitahidi kurahisisha upatikanaji wa matokeo kuanzisha njia mbalimbali za kuangalia. Wanafunzi, wazazi, na wadau wote wa elimu sasa wanaweza kutumia njia hizi kupata taarifa muhimu kuhusu matokeo haya kwa haraka na urahisi.
Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 Kupitia Mtandao (Online)
Njia rahisi na inayopendelewa na wengi ni kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita 2024 kupitia mtandao. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hutoa matokeo haya kwenye tovuti yao rasmi. Ili kuangalia matokeo yako, fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti ya NECTA: Fungua kivinjari chako cha intaneti (kama vile Google Chrome, Mozilla Firefox, au Safari) na uandike anwani ya tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz) kwenye kisanduku cha anwani. Kisha, bonyeza “Enter” ili kuingia kwenye tovuti.
- Nenda kwenye menyu ya matokeo: Kwenye ukurasa wa nyumbani wa tovuti ya NECTA, tafuta sehemu iliyoandikwa “Results”. Bonyeza sehemu hiyo ili kuendelea.
- Chagua Matokeo ya ACSEE: Katika ukurasa wa matokeo, utaona chaguo mbalimbali za mitihani. Chagua “Matokeo ya ACSEE” ili kuonyesha matokeo ya Kidato cha Sita.
- Chagua mwaka wa matokeo: Baada ya kuchagua “Matokeo ya ACSEE,” utaona chaguo la miaka tofauti ya mitihani. Chagua “Matokeo ya ACSEE 2024” ili kuona matokeo ya mwaka 2024 pekee.
- Tafuta shule yako: Kwenye ukurasa unaofuata, utaona orodha ya shule zote zilizofanya mtihani wa Kidato cha Sita. Tumia kisanduku cha kutafutia (search box) ili kuandika jina la shule yako na ubofye “Enter” au “Search.”
- Fungua kiungo cha shule yako: Baada ya kupata jina la shule yako, bonyeza kiungo chake ili kuona matokeo ya wanafunzi wa shule hiyo.
- Tafuta jina lako: Kwenye ukurasa wa matokeo ya shule yako, tafuta jina lako kwa makini.
Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Kupitia USSD
Kwa wale ambao hawana urahisi wa kutumia intaneti, NECTA imetoa njia ya kuangalia matokeo kupitia SMS. Njia hii ni rahisi na ya haraka, na inahitaji tu kuwa na simu ya mkononi yenye uwezo wa kutuma na kupokea ujumbe mfupi. Ili kuangalia matokeo yako kupitia SMS, fuata hatua zifuatazo:
- Piga *152*00#: Fungua sehemu ya kupiga simu kwenye simu yako na piga namba *152*00#. Kisha utaona orodha ya huduma mbalimbali kwenye skrini ya simu yako.
- Chagua Elimu: Kutoka kwenye orodha, chagua namba 8 (ELIMU) kwa kutumia vitufe vya simu yako.
- Chagua NECTA: Baada ya kuchagua “Elimu,” utaona orodha nyingine ya huduma. Chagua namba 2 (NECTA).
- Chagua Matokeo: Kwenye orodha inayofuata, chagua namba 1 (MATOKEO).
- Chagua ACSEE: Utaona orodha ya aina za mitihani. Chagua namba 2 (ACSEE) kwa kuwa unataka kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita.
- Andika namba ya mtihani na mwaka: Sasa, andika namba yako ya mtihani (index number) pamoja na mwaka wa mtihani. Kwa mfano, kama namba yako ya mtihani ni S0334-0556 na mwaka wa mtihani ni 2024, andika S033405562024.
- Chagua aina ya malipo: Utaombwa kuchagua jinsi ya kulipa gharama ya huduma hii. Kawaida, gharama huwa ni Tshs 100/= kwa kila SMS. Chagua njia ya malipo inayokufaa zaidi.
- Pokea matokeo: Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi (SMS) wenye matokeo yako ya Kidato cha Sita 2024.
Leave a Comment