Kuangalia Salio la Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS
- Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
- Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Balance” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Balance 123456789.
- Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.
Kupata Taarifa ya Statement ya Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS
- Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
- Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Statement” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Statement 123456789.
- Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.
Jinsi ya Kuangalia Salio La NSSF WhatsApp
- Hifadhi namba 0756 140 140 kwenye simu yako.
- Fungua WhatsApp na tuma ujumbe “Hello” au “Habari”.
- Fuata maelekezo ili kuangalia salio lako (“Balance”) au taarifa za michango (“Statement”)
Jinsi ya Kuangalia Salio la NSSF kwa Programu ya Simu Janja
- Pakua programu ya “NSSF Taarifa” kutoka Google Play Store.
- Ingia kwa kutumia maelezo yako ya NSSF.
- Angalia salio lako, michango, na taarifa nyingine muhimu.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
- Salio unalopokea kwa njia ya simu linaweza kuwa tofauti kidogo na lile utakalopewa moja kwa moja kwenye ofisi za NSSF. Hii ni kwa sababu kunaweza kuwa na mabadiliko madogo ambayo hayajaingizwa kwenye mfumo wa simu bado.
Leave a Comment