MASHARTI YA MAREKEBISHO YA MAJINA
Maombi ya marekebisho yawasilishwe katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja baada ya matokeo ya mtihani kutolewa.
Marekebisho ya jina ni lazima yawe na lengo la kufanya jina linalohitajika lifanane na jina lililotumika katika mtihani wa sifa (awali).
Marekebisho yanayokusudia kuongeza jina jipya au kuondoa/kubadilisha jina (Mfano: Magina kuwa
Madoba) hayaruhusiwi.
- Marekebisho yanayolenga kuboresha herufi zisizoathiri Matamshi ya jina linapotamkwa yanaweza kuombwa kufanyika.
- Msingi pekee wa marekebisho ya jina ni mtihani wa sifa (awali) na sio jina lililopo katika viapo vya mahakama, vyeti vya ndoa, ubatizo n.k.
- Cheti halisi chenye jina lilikosewa ni lazima kirudishwe NECTA kwa ajili ya mchakato wa marekebisho.
HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAOMBI
1. Fungua tovuti (Website) ya NECTA (www.necta.go.tz)
2. Chagua na ubonyeze huduma mtandao (E-services), halafu chagua (Replacement Certificate)
3. Bonyeza “Generate Control Number” ili kupata nambari ya malipo (Control Number)
4. Ingiza taarifa zako kama hapa chini ili kupata: Control Number”

5. Bonyeza “save” baada ya kujaza taarifa zako kwa usahihi.
6. Lipia ada ya marekebisho ya jina ya Tsh.35, 000/= (kwa cheti kimoja) kupitia benki au mitandao ya simu kwa kutumia ‘Control number’ uliyotengeneza.
Baada ya kufanya malipo
7. Bonyeza Marekebisho ya Majina (Correction of Names) na ufanye maombi (Apply/New)
8. Ingiza nambari ya simu ya mkononi na nambari ya malipo (Control Number).
9. Jaza fomu ya maombi mtandao (Online Application Form) kisha Wasilisha ombi kwa kubofya ‘Submit’.
MAJIBU
Baada ya marekebisho kufanyika, Hati ya Matokeo (Results Slip) au cheti kipya chenye marekebisho kitatumwa kwa mkuu wa shule au kwa mtahiniwa (endapo si mwanafunzi).
Mawasiliano
Eneo la Viwanda Mikocheni, Barabara ya Bagamoyo,
S.L.P. 2624 au 32019 DAR-ES-SALAAM TANZANIA
Simu: +255-22 2700493-6/9 +255-22-2772423
Nukushi: +255-22-2775966
Barua pepe: esnecta@necta.go.tz,
Tovuti: www.necta.go.tz
Leave a Comment