Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Jinsi ya Kuhakiki Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo Online 2025/2026

Jinsi ya Kuhakiki Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo Online 2025/2026

MUONGOZO WA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO

Uhakiki unafanyika kupitia mfumo wa eRITA pekee. Walio na VYETI VYA ZAMANI vilivyochapwa kwa typewriter watalazimika kwanza kupata vyeti vya kidijitali kwa kufuata hatua namba 1-6 hapo chini na baada ya hapo achague OLD to NEW. Baada ya kukamilisha hatua hiyo na kupata cheti kipya ataendelea na uhakiki.

Waombaji wote wanatakiwa kufuata muongozo ufuatao;

1. Ingia kwenye tovuti ya Wakala www.rita.go.tz;

2. Bonyeza kitufe kilichoandikwa eRITA;

3. Chagua Huduma ya Vizazi na Vifo;

4. Bonyeza REGISTER katika kipengele cha REGISTRATION na jaza taarifa zote kwa usahihi kufungua akaunti ya maombi; (Muhimu: Nenosiri (Password) liwe na herufi zaidi ya nane ikiwa na mchanganyiko wa herufi kubwa na alama mojawapo (mfano @#$” !* &),

5. Ingia katika akaunti ya barua pepe “email” fungua ujumbe uliotumiwa kutoka RITA kisha bonyeza neno “Account activation

6. Ingia tena katika mfumo wa eRITA na bonyeza kitufe cha SIGN IN na jaza taarifa ili katika mfumo;

7. Chagua BIRTH SERVICES kwa huduma ya Kizazi /(DEATH SERVICES kwa huduma ya kifo) Kisha bonyeza alama ya jumlisha upande wa chini kulia.

8. Chagua REQUEST VERIFICATION na jaza taarifa zote kwa usahihi ikiwa pamoja na namba ya cheti cha kuzaliwa au kifo (namba hii ipo katika safu (column) namba moja (1 ) katika cheti);

9. Thibitisha taarifa ulizojaza kisha chagua kitufe cha kwenda mbele;

10. Fanya malipo sahihi kulingana na ankara uliyopata kwenye mfumo;

11. KUPATA MAJIBU YA UHAKIKI: Ingia katika akaunti uliyofungua ya mfumo wa eRITA, chagua huduma ya BIRTH/DEATH ->Submitted->Details. Mfumo ukionesha neno verified itamaanisha cheti chako ni halali. Pakua (Download) fomu ya uthibit- isho utakayotumia kupata huduma unayohitaji.

Kwa waombaji wa huduma za NHIF na HELSB watajaza namba ya ombi inayopatikana kwenye fomu upande wa juu kulia.

Leave a Comment