Umewahi kufikiria majibu sahihi endapo mwajiri wako akikuuliza “Unahitaji tukulipe kiasi gani?” (How much do you want us to pay you?). Hili swali ni la mtego na limekaa kitaalamu sana kupima uwezo wa kufikiri wa mtu anayehojiwa.
Taasisi nyingi mishahara ni fixed (zina salary scales ambazo si rahisi kubadilishwa na bargaining power yako kwenye interview). Fanya utafiti kwanza; uliza watu. Mishahara kwenye taasisi nyingi inafahamika.
Mfano 1: “Based on commitment, hardwork and dedication I am expecting to offer to this job 1.2M would be an acceptable amount“
Unaweza kujibu kwa makadirio (I’m expecting my salary to fall between …)
Mfano 2: “I am seeking a position that pays between Tsh 2.5M and Tsh 5M annually.”
Kwanini hili swali huulizwa?
Sababu ni kadhaa;
– Mwajiri anatamani kujiridhisha kama anao uwezo wakufikia matarajio yako ya kimaslahi
– Kujua thamani yako
– Kuweka makubaliano ya awali ya kiasi gani utalipwa
– Kujua kama ulifanya utafiti wa kujua mwajiri anatarajia kukulipa kiasi gani, nk.
Hitimisho
Wapo baadhi ya wasailiwa wanaosema “mshahara wowote“. Don’t fall into that trap. Ni kiashiria cha unyonge na kutokujua thamani yako au kuonesha kuwa wewe si bidhaa bora sokoni.
Leave a Comment