Je umewahi kukutana na swalin la “What is your weakness?” katika interviw/usaili? kama hujakutana nalo basi jiandae kama unampango wa kufanya usaili wa kutafuta kazi au fursa yoyote popote.
What is your weakness?/What are your weaknesses? Swali hili limekaa kimtego, ni kama unaambiwa tupe sababu kwa nini tusikuajiri 😁. Hilo siyo lengo lake lakini ukijichanganya waweza mpa mwajiri sababu ya kukutema.
Katika kujibu swali hili wapo watu wa aina mbili. Aina ya kwanza, wanaoshawishika kusema “I don’t have any” kitu ambacho ni unrealistic and unconvincing.
Na ukijibu hivi ni ishara kwamba wewe si muwazi. Aina ya pili, wanajibu swali hili kuonesha sifa nzuri ila wanaiwasilisha kwa namna hasi ionekane kama udhaifu. Mathalani mtu anasema “mimi udhaifu wangu ni kufanya kazi kupita kiasi mpaka wkt mwingine napitiliza masaa ya kazi”. Bado sidhani kama hii ni njia bora pia. Unaweza onekana kabisa unawapiga kamba watu wazima. Ninashauri kuchagua weakness yako ya kweli kabisa lakini si ile inayoweza athiri utendaji wako kazini au kupunguza chance ya kupata kazi.
Kumbuka, mtu makini ni yule anayeonesha jitahada kurekebisha madhaifu yake anapoyagundua hivyo ukishaitaja iambie panel your efforts to rectify it.
Kwa mfano (Post ya legal officer): One of weaknesses is computer programming. I have been curious to know how it is done but it has never been easy for me; I especially struggle with coding. I have been trying to learn from my friends who are IT experts and I think I am getting better slowly but surely. Katika jibu hili utagundua weakness ya computer programming skills haziwezi kuathiri utendaji wa legal officer so it is not a big deal.
Katika majibu yako angalia usijejiua kwa kuanza kusema kwamba udhaifu wako ni uzembe, uvivu, uaminifu, nk. utajikaanga. Kumbuka swali hili linaweza ulizwa kivingine mfano “If you could change one thing about yourself, what would it be?”
Leave a Comment