Zifuatazo ni hatua za kukata tiketi ya treni ya mwendokasi ya sgr kwa njia ya mtandao
Hatua ya 1: Tembelea Tovuti ya Ukataji wa Tiketi ya Treni
Anza safari yako ya kununua tiketi ya treni mtandaoni kwa kutembelea tovuti rasmi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ya mfumo wa mfumo wa kukata tiketi ya Treni (eticketing.trc.co.tz) ni https://eticketing.trc.co.tz/.
Hatua ya 2: Jaza Taarifa za Safari
Kwenye tovuti, chagua kituo unachotoka na kituo unachokwenda. Bainisha idadi ya wasafiri watakaokuwa kwenye safari hiyo, ikiwemo watoto (wenye umri wa miaka 4-12) au watoto wachanga (wenye umri wa miaka 0-3) watakaosafiri nawe. Baada ya kujaza taarifa hizo, bofya kitufe cha “Fanya Uhifadhi” ili kuendelea.
Hatua ya 3: Chagua Treni
Katika hatua hii, utaona orodha ya treni zinazopatikana kwa safari yako iliyochaguliwa. Hakikisha umechagua treni sahihi inayokwenda unakoelekea kwa kubofya kitufe cha “Chagua” kisha uendelee mbele.
Hatua ya 4: Chagua Siti
Baada ya kuchagua treni, utaelekezwa kuchagua behewa la daraja unalotaka kusafiria. Chagua siti au kitanda kulingana na idadi ya wasafiri uliowekata awali. Kisha bofya kitufe cha “Endelea Mbele.”
Hatua ya 5: Jaza Taarifa za Wasafiri
Katika sehemu hii, jaza taarifa sahihi za wasafiri wote watakaokuwa kwenye safari. Hakikisha unaweka taarifa sahihi za vitambulisho kwa wasafiri wazima. Pia, weka taarifa za mawasiliano ikiwemo namba ya simu au barua pepe ambayo inaweza kutumika kwa urahisi.
Hatua ya 6: Thibitisha Taarifa
Kabla ya kuendelea, hakikisha taarifa zote ulizoweka ni sahihi, ikiwemo maelezo ya treni, siti/kitanda, taarifa za wasafiri, na nauli ya safari. Ukishajiridhisha, bofya kitufe cha “Fanya Uhifadhi” ili kukamilisha hatua hii.
Hatua ya 7: Fanya Malipo
Mara tu utakapokamilisha uhifadhi, utapokea ujumbe mfupi wa simu (SMS) wenye maelekezo ya jinsi ya kufanya malipo. Unaweza kulipia kwa kutumia simu yako ya mkononi au kwa kutembelea wakala wa TRC.
Leave a Comment