Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma 2025/2026

Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma 2025/2026

Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma

Mtumishi anapohitaji kibali cha Uhamisho kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa kwenda TAMISEMI anapaswa kuwa na vitu vifuatavyo:-

1. Barua ya kumuombea kibali iliyoandikwa na Mwajiri wake (Mkurugenzi)

2. Barua yake ya maombi ya uhamisho aliyotuma kule anakotaka kuhamia

3. Barua ya kukubaliwa maombi yake ya uhamisho kutoka kwa Mwajiri wa mahali anakotaka kuhamia

4. Barua yake ya ajira

5. Barua ya kuthibitishwa kazini

6. Nakala ya kitambulisho cha kazi

7. Nakala ya hati ya mshahara(Salary slip)

8. Kiambatisho cha sababu ya kuhama kwake ( kama ni kumfuata mwenza lazima awe na cheti cha ndoa, kama ni kwa sababu za kifamilia kwamfano kuwa karibu na wazazi au ndugu zake wanaomtegemea anapaswa kuwa na barua ya Mtendaji wa Kata/kijiji/Mtaa wa kule anakokwenda, kama ni ugonjwa barua ya Rufaa/au ya Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Serikali inayoonesha kuwa mtumishi anahitaji kupata matibabu katika Hospitali ya mahali anakoomba kuhamia, ikiwa ni kubadilishana taarifa za mtumishi mwenzake wanayebadilishana naye ).

Leave a Comment