Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018 kwa lengo la kutoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Majukumu ya Mfuko
- Kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na isiyo rasmi
- Kukusanya michango
- Kuwekeza
- Kulipa mafao
Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama wa NSSF aliyepoteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira yake imefika ukomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (resignation).
Jinsi ya Kupata Mafao ya kupoteza ajira kwa mwanachama wa NSSF
Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama mwenye sifa zifuatazo
1. Mwanachama awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na nane (18)
2. Awe mwanachama wa NSSF aliye poteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira imefikia kikomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation)
3. Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
4. Asiwe na sifa ya kulipwa mafao ya muda mrefu ambayo ni Pensheni ya uzee, Ulemavu au urithi/wategemezi
5. Ithibitishwe kuwa mwanachama hayupo kwenye ajira yoyote Awe na umri chini ya miaka 55.
Leave a Comment