Fahamu Jinsi ya Kupata Mafao ya Kustaafu NSSF. Mfuko la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hutoa mafao ya pensheni ya uzee ambayo hulipwa kila mwezi kwa mwanachama aliyetimiza sifa zifuatazo:
- Awe ametimiza umri wa kustaafu kwa hiari kuanzia umri wa miaka 55 mpaka 59 au kustaafu kwa lazima kwa umri wa miaka 60
- Awe amechangia katika mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa kipindi kisichopungua miezi (180)
Malipo ya pensheni ya uzee hulipwa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo
- Mshahara wa mwanachama
- Idadi ya michango kwenye Mfuko na
- Kiwango cha kukuza michango (accrual rate)
Malipo yatolewayo kama Mafao ya uzeeni ni kama yafuatayo
Kwa wanachama waliostaafu kuanzia tarehe 1 Julai 2022
- Mkupuo wa awali kabla ya kuanza malipo ya pensheni ambayo ni sawa na asilimia 33% ya pensheni ya mwaka mara 12.5
- Pensheni ya kila mwezi
- Mkupuo maalum kwa mwanachama aliyekosa sifa ya pensheni yaani jumla ya michango ya mwanachama pamoja na riba
Namna ya kukokotoa pensheni ya uzee/ Kanuni ya Pensheni ya uzee
A.Kanuni ya malipo ya mkupuo
1/580 x N x APE x 12.5 x 33%
1/580 =Kiwango cha kukuza michango (accrual rate)
N =Idadi ya miezi ya kuchangia
APE=Mshahara wa mwaka unaopatikana kwa kutafuta wastani wa mishahara mikubwa ya miaka mitatu katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho ya uanachama
12.5=Kiwango kinachozidisha malipo ya pensheni kuwa mkupuo kabla yamalipo ya pensheni ya kila mwezi
33%=Asilimia ya kiwango cha malipo ya pensheni kwa mkupuo
B.Kanuni ya Malipo ya Pensheni ya Uzee ya Kila Mwezi
1/580 x N x APE x 67% x 1/12
1/580 = Kiwango kinachokuza michango (accrual rate)
N = Idadi ya miezi ya kuchangia
APE = Mshahara wa mwaka (wastani wa mishahara mikubwa ya miaka mitatu katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho)
67%= Kiwango cha malipo ya Pensheni baada ya kuchukua mkupuo wa asilimia ishirini na tano (33%).
Kwa wanachama waliostaafu kipindi cha nyuma mpaka tarehe 30 Juni 2022
- Mkupuo wa awali kabla ya kuanza malipo ya pensheni ambayo ni sawa na asilimia 25% ya pensheni ya mwaka mara 12.5
- Pensheni ya kila mwezi
- Mkupuo maalum kwa mwanachama aliyekosa sifa ya pensheni yaani jumla ya michango ya mwanachama pamoja na riba
Namna ya kukokotoa pensheni ya uzee/ Kanuni ya Pensheni ya uzee
A.Kanuni ya malipo ya mkupuo
1/580 x N x APE x 12.5 x 25%
1/580 =Kiwango cha kukuza michango (accrual rate)
N =Idadi ya miezi ya kuchangia
APE=Mshahara wa mwaka unaopatikana kwa kutafuta wastani wa mishahara mikubwa ya miaka mitatu katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho ya uanachama
12.5=Kiwango kinachozidisha malipo ya pensheni kuwa mkupuo kabla yamalipo ya pensheni ya kila mwezi
25%=Asilimia ya kiwango cha malipo ya pensheni kwa mkupuo
B.Kanuni ya Malipo ya Pensheni ya Uzee ya Kila Mwezi
1/580 x N x APE x 75% x 1/12
1/580 = Kiwango kinachokuza michango (accrual rate)
N = Idadi ya miezi ya kuchangia
APE = Mshahara wa mwaka (wastani wa mishahara mikubwa ya miaka mitatu katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho)
75%= Kiwango cha malipo ya Pensheni baada ya kuchukua mkupuo wa asilimia ishirini na tano (25%).
Leave a Comment