Fahamu Jinsi ya Kupata Mafao ya Kuacha/Kuachishwa NSSF kwa Haraka (Utaratibu). Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama wa NSSF aliyepoteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira yake imefika ukomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation).
Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama aliyetimiza vigezo vifuatavyo;
- Mwanachama awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na nane (18)
- Awe mwanachama wa NSSF aliye poteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira imefikia kikomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation)
- Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Asiwe na sifa ya kulipwa mafao ya muda mrefu ambayo ni Pensheni ya uzee, ulemavu au urithi/wategemezi
- Ithibitishwe kuwa mwanachama hayupo kwenye ajira yoyote
- Awe na umri chini ya miaka 55.
Ukomo wa Mafao ya Kupoteza Ajira
Iwapo mwanachama ataendelea kukosa ajira baada ya kuisha kwa kipindi cha miezi 18, anaweza kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi Mkuu ili baki ya michango yake ihamishiwe kwenye mpango wa uchangiaji wa hiari atakaouchagua mwenyewe ili aendelee kuchangia kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mpango husika.
Tahadhari
Ni kosa la jinai chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018, kwa mtu yeyote kwa makusudi kutoa taarifa za uongo/ zisizo sahihi kwa lengo la kujipatia mafao yeye mwenyewe au mtu mwengine.
Fata hatua hizi kupata mafao yako ya NSSF
1. Chukua hiyo barua ya kuacha/kuachishwa kazi
2. Nenda tawi lolote la NSSF, utapewa fomu ya viambatanisho (picha tatu, NIDA, bank statement na hiyo barua) Ndani ya siku 15 mpaka mwezi unapewa mpunga wako.
Kumbuka
Mwanachama atalipwa asilimia 33.3 ya mshahara wake aliokuwa anapata wakati akiondoka kwenye ajira. Malipo hayo yatalipwa kwa kila mwezi mfululizo kwa kipindi kisichozidi miezi sita ndani ya mwaka mmoja. Malipo ya kila mwezi yatakoma iwapo mwanachama atapata ajira
Mwanachama ambaye atakuwa hajatimiza michango ya miezi 18 atalipwa mkupuo wa asilimia hamsini (50%) ya jumla ya michango yake.
Leave a Comment