Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu
Kupata namba ya NIDA kumekuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali. Sasa mtu yeyote anaweza kupata namba ya NIDA kwa urahisi na haraka kupitia simu ya mkononi, bila kujali mahali alipo au aina ya simu anayotumia. Hadi hivi sasa kuna njia kuu mbili za kupata namba ya NIDA kwa kutumia simu ya mkononi. Njia hizi ni kama zifuatazo;
- Kupitia USSD: Huu ni mfumo unaokuwezesha kuingiliana na kompyuta ya NIDA kwa kutumia misimbo maalumu. Ni njia rahisi na ya haraka ambayo haihitaji muunganisho wa intaneti.
- Kupitia SMS: Njia hii inahusisha kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba maalum ya NIDA. Kama ilivyo kwa USSD, njia hii pia haihitaji muunganisho wa intaneti.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSSD
USSD (Unstructured Supplementary Service Data) ni njia rahisi na ya haraka ya kupata namba ya NIDA bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. Fuata hatua hizi rahisi:
- Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
- Chagua namba 2 (NIDA).
- Ingiza majina yako matatu (3) uliyojisajili .
- Ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi
- Kubali ombi lako.
- Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Leave a Comment