Kuna njia mbalimbali unazoweza kutumia kupata namba yako ya NIDA mtandaoni, bila kujali unatumia simu ya kawaida au simu janja. Zifuatazo ni njia kuu za kupata namba yako ya NIDA:
1. Kupitia Tovuti Rasmi ya NIDA
Hatua za kufuata:
- Fungua kivinjari kwenye simu yako au kompyuta na utembelee tovuti rasmi ya NIDA kwa kubofya hapa au https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin.aspx.
- Jaza taarifa unazohitajika, ikiwa ni pamoja na:
- Jina la Kwanza
- Jina la Mwisho
- Tarehe ya Kuzaliwa
- Jina la Kwanza la Mama
- Jina la Mwisho la Mama
- Baada ya kujaza taarifa hizi, thibitisha kuwa wewe sio roboti kwa kuingiza neno unaloonyeshwa kwenye picha.
- Bofya kitufe cha Angalia ili kupata namba yako ya NIDA.
2. Kupata Namba ya NIDA kwa USSD
Kama huna simu janja au huwezi kupata intaneti, unaweza kupata namba yako ya NIDA kwa kutumia USSD kwenye simu yako ya kawaida. Fuata hatua hizi:
- Piga *152*00# kwenye simu yako.
- Chagua Ajira na Utambuzi kwa kubonyeza namba 3.
- Chagua NIDA kwa kubonyeza namba 2.
- Ingiza majina yako matatu uliyojisajili (mfano: Dan John Sele).
- Ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi ya NIDA.
- Thibitisha maombi yako na subiri ujumbe mfupi (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Leave a Comment