Fahamu jinsi ya kulinda WhatsApp yako isiweze kuhakiwa. Kuna njia nyingi ambazo zinaweza kutumia kuhaki WhatsApp za watu, ambazo ma hackers hutumia. Hackers wengi kwa kipindi cha hivi karibuni wamekuwa wakidukua akaunti za watu na kusambaza jumbe za kampeni za kitapeli mfano. Kupata pesa bure UNCEF n.k.
Tumekuletea makala fupi ambayo utajifunza jinsi ya kulinda WhatsApp yako isiweze kuhakiwa na mtu yoyote. Kwa Njia hii utajifunza jinsi ya kulinda WhatsApp yako isiweze kuhakiwa kiurahisi.
Tumia njia hii ili kuiokoa account yako ya WhatsApp.
1. Ukiwa kwenye page ya WhatsApp bonyeza *settings*
2. Kisha bonyeza *account*
3. Bonyeza *two-step verification*
4. Bonyeza *Turn ON*
5. Kisha chagua *PIN* na pia unaweza kuweka e-mail yako.
Two step verification inachofanya ni kuongeza ulinzi, mtu aki hack account yako hataweza kuitumia bila kuwa na PIN. Labda umpe wewe na PIN yako. Ukiweka na E-mail itakuwa rahisi kuirudisha account yako bila ya madhara ya aliyefanikiwa ku hack account yako kuweza kuwasumbua au hata kuwaibia watu wengine.
Kumbuka:
Namba au ujumbe wowote unaoingia katika simu yako kwa kupigiwa au SMS ukiwa na code usimpe mtu, endapo atakupigia au kukutumia SMS kuomba hizo code usitoe hata akitoa sababu ya aina yoyote.
Leave a Comment