TANGAZO LA KUONGEZA MUDA WA KUOMBA AJIRA.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji tarehe 13 Februari, 2025 lilitoa tangazo la nafasi za ajira ambapo mwisho wa kuwasilisha maombi hayo ilikuwa 28 Februari, 2025. Jeshi linautangazia umma kuwa zimeongezwa siku saba (7) hivyo, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya nafasi ya ajira ni tarehe 07 Machi, 2025 badala ya 28 Februari, 2025. Aidha, vijana wenye sifa na nia ya kujiunga na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waendelee kutuma maombi.
Maombi yote yatumwe kupitia link: ajira.zimamoto.go.tz. Maelezo mengine ni kama yalivyosomeka katika tangazo la tarehe 13 Februari, 2025.

Leave a Comment