KUCHUKUA KITAMBULISHO KATIKA OFISI YA NIDA YA WILAYA YAKO
Kufuatia baadhi ya wananchi kutochukua Vitambulisho vyao vilivyokuwa katika ofisi za Kata, Vijiji, Mitaa na Shehia, Vitambulisho hivyo sasa vimekusanywa na kurudishwa katika ofisi za NIDA za Wilaya
Ukipokea Ujumbe Mfupi wa simu (SMS) fika ofisi ya NIDA Wilaya uliko jisajili kuchukua Kitambulisho chako.
Kumbuka
Atakayeshindwa kuchukua Kitambulisho chake ndani ya mwezi mmoja toka kupokea ujumbe mfupi wa simu, matumizi ya Namba yake ya Utambulisho wa Taifa (NIN) yatasitishwa.

Leave a Comment